Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amesema wamejipanga kuhakikisha wanafanya tamasha la utamaduni la Kitaifa ambalo ni kubwa kuwahi kutokea, litakalojumuisha mikoa yote nchini kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa ushindani, ambapo mkoa mshindi utakuiwa mwenyeji wa tamasha kwa mwaka unaofuata.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo wakati akisoma hotuba yake ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka 2024-2025 leo Bungeni Jijini Dodoma na kudai kuwa lengo ni kufikia kila mtaa nchini kuibua, kulea na kupatia jukwaa la kutangaza na kujitangaza kwa kuwaunganisha wasanii na masoko makubwa ya Kimataifa kisanaa.

Amesema, “hii itaibua chachu ya kukuza na kulinda tamaduni zetu Nchini lakini pia Kufungua vituo 100 vya ufundishaji Kiswahili kote Duniani kwa kushirikiana na Diaspora, lengo ni kukuza, kueneza na kubidhaisha zaidi Kiswahili, Kukuza sanaa mtaa kwa mtaa kupitia programu ya BASATA Vibes.”

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro.

Kuhusu bajeti, Dkt. Ndumbaro amesema, hadi kufikia Aprili, 2024 bajeti ya mwaka 2023/24 imeongezeka na kufikia Shilingi Bil. 48,348,827,89 ikiwa ni ongezeko la Shilingi Bil. 12,903,786,895 na kwamba Aprili, 2024 Wizara pia ilipokea Shilingi Bilioni 40,487,566,685 sawa na asilimia 83.7 ya bajeti yote iliyotengwa mwaka wa fedha 2023/24.

“Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 7,654,889,768 ni Mishahara ambayo ni sawa na asilimia 79 ya bajeti ya mishahara, Shilingi Bilioni 19,284,302,010 ni Matumizi Mengineyo na Shilingi Bilioni 13,548,374,907 ni Miradi ya Maendeleo, sawa na asilimia 78 ya bajeti ya Miradi ya Maendeleo.

TIRA: Msisaini mikataba kama hamjaielewa
Wananchi Malinyi wapata tumaini jipya la mawasiliano