Serikali imetoa Shilingi Milioni 800 kwa ajili ya ukarabati wa barabara za Igawa – Malinyi, Lugala – Misegese, Njiapanda – Malinyi zilizoathiriwa na mto furua na kuharibu barabara inayohudumiwa na TANROADS pamoja na zile zinazohudumiwa na TARURA kitu kilichosababisha Wananchi wa Malinyi kukosa mawasiliano.
Akikagua uharibifu huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amejiridhisha kuwa miundombinu hiyo imeharibiwa na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni na kudai kuwa fedha za dharura zipelekwe haraka kurejesha mawasiliano ya barabara ya Kichangani.
Aidha, amemuagiza Meneja wa Wakala ya Barabara Mijini na Vijijini – TARURA, Mkoa wa Morogoro Injinia Emmanuel Ndyamukama kutangaza zabuni hiyo ndani ya wiki na mkandarasi atakayepatikana aanze kujenga barabara hiyo haraka huku mawasiliano yakiendelea kufanyika na Wizara ya Ujenzi ili kuona namna ya kujenga Daraja la Mto Furua lilichukuliwa na maji na kukata mawasiliano ya barabara hiyo.
Amesema, ‘nimeshawaelekeza watendaji wa Wizara yangu Naibu Katibu Mkuu anayesimamia miundombinu ambaye ndiye anayewasimia TARURA kuleta fedha hizo kwa Meneja wa TARURA mkoa amesema wanahitaji Mil. 800, nimewapa wiki mbili nataka Barabara hii ipitike.’’
Hata hivyo, amewataka viongozi wa ngazi zote kushirikiana na kuwa wabunifu ili kuwatumikia wananchi kikamilifu huku akiwaagiza Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara kuitisha vikao vya dharura na wataalamu wote ndani ya Mikoa yao pamoja na wadau wa Maendeleo

Wizara kuratibu tamasha la Utamaduni la Kitaifa
Mlipuko Kiwandani wauwa 11 Mtibwa