Mhubiri wa Kanisa la Good News International lililopo kaunti ya Kilifi Malindi, Paul Mackenzie, mkewe Rhoda Mackenzie na watuhumiwa wengine 16 wanatarajiwa kuwasilishwa hii leo katika mahakama ya Shanzu.

Mackenzie na wafuasi wake hao akiwemo mkewe wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya ugaidi baada ya mahakama ya Malindi Kaunti ya Kilifi kuwawachilia huru na kisha kukamatwa tena.

Mchungaji Paul Mackenzie na Watuhumiwa wengine wakiwa katika ukumbi wa Mahakama.

Jana Mei 4, 2023 Mhubiri mwingine mashuhuri nchini humo, Ezekiel Odero aliachiliwa kwa dhamana na Mahakama ya Shanzu mjini Mombasa na atakuwa akiripoti mara moja kwa juma kusubiri uchunguzi dhidi ya tuhuma za kuhusishwa na vifo vya watu zaidi ya 100 kwa kushirikiana na Mackenzie.

Odero pia atakuwa akisubiri rufa aliyoikata ya kutaka huduma za Kanisa lake zilizozuiliwa ziweze kuendelea na Sreikali iondoe zuio la akaunzi zake za Benki ilizozifunga.

Azam FC yaanza safari ya Mtwara
Tanzania yajivunia mazingira bora uwekezaji sekta ya Afya