Zaidi ya Wagonjwa 5000 wa nchi zinazoizunguka Tanzania huja nchini kupata huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kila mwaka, kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika eneo la miundombinu, vifaa tiba na Watumishi wenye ujuzi mkubwa.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa ziara yake ya katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ambapo pia alipata fursa ya kuongea na Watumishi wa Afya.

Amesema, “watu wanaotoka Nje ya Nchi zinazotuzunguka kwa mwaka kuja kupata huduma za kibingwa na kibingwa bobezi ni zaidi ya 5000, kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Sekta ya Afya.”

Serikali ya Tanzania tayari imesaini mikataba na nchi za Zambia, Malawi kwa ajili ya kuleta Wagonjwa wao nchini kupata huduma za kibingwa na ubingwa bobezi na kwamba imepunguza asilimia 97 ya Wagonjwa kwenda kupata matibabu nje ya Nchi.

Kenya: Mchungaji Mackezie kupandishwa kizimbani hii leo
Hii hapa hatma ya timu za majeshi Ligi Kuu