Wakati Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kipaumbele chake ndani ya timu hiyo kwa sasa ni kuonyesha soka safi na la kuvutia, uongozi wa timu hiyo umeweka wazi utakuja kivingine katika msimu ujao, imefahamika.

Kauli hiyo imetolewa baada ya kikosi chao kuonyesha kandanda safi iliyoonyeshwa kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting, iliyomalizika kwa ushindi wa mabao 3-0.

Robertinho amesema ni jambo jema ni kucheza soka safi na kupata ushindi mnono kwa sababu inaongeza furaha kwa mashabiki.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil amesema mechi ilikuwa ngumu katika kipindi cha kwanza kutokana na wapinzani wao, Ruvu Shooting kucheza vizuri na kutengeneza nafasi ambazo walishindwa kuzitumia baada ya nyota wa Simba kufanya makosa.

Ameongeza aina yake ya ushangiliaji katika mabao ya juzi alikuwa anajaribu kuwapa furaha mashabiki waliojitokeza pamoja na kupitia kipindi kigumu.

“Nimefurahi ushindi wetu dhidi ya ruvu Shooting kwa sababu mbili, tumecheza vizuri halafu tumepata mabao mengi, hilo ndio kubwa, kuhusu nilivyokuwa nashangilia nilikuwa nawafurahisha mashabiki ambao walikuwa wakiniambia nicheze,” amesema Robertinho.

Simba SC inaendeleea kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa mwishoni mwa juma hili katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es salaam.

Jeshi wapiga marufuku uchoraji wa tattoo mwilini
Waliopanga kumpindua Rais watupwa Gerezani