Msemaji wa Ikulu ya Chad, Brah Mahamat amesema watu 11 wanaoshutumiwa kupanga mapinduzi nchini humo wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, huku Rais wa Chad, Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno akisema watasamehewa.

Watu hao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Shirika la kutetea haki za binadamu la Chad – OTDH, na mkosoaji mkubwa wa utawala, Berdei Targuio wamezuiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali la Koro Toro, lolilopo umbali wa kilomita 600 eneo la kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, D’jamena.

Rais wa Chad Jenerali Mahmat Idriss Deby Itno.

Kifungo hicho cha miaka 20, kimetolewa dhidi yao wakidaiwa kuvunja utaratibu wa kikatiba, kumiliki silaha kinyume cha sheria na kushirikiana na wahalifu kupanga mpango huo wa kufanya mapinduzi mwezi Desemba.

Deby alichukuwa madaraka baada ya baba yake, Idriss Deby Itno, aliyetawala kwa miaka 30 kufariki wakati wa operesheni dhidi ya waasi Aprili, 2021 ambaye alisema ni lazima hukumu itangazwe kabla ya kuwaachilia huru.

Soka safi lamridhisha Kocha Simba SC
Tetesi mlipuko mpya Uviko-19: Wizara yatoa kauli