Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema asilimia 94.4 ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU), wanatambua hali zao na kati yao asilimia 98.8 wanatumia dawa za kufubaza makali ya VVU na Ukimwi.

Ummy ameyasema hayo hii leo Mei 12,2023 bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo, ambapo amesema pia asilimia 96.6 ya Waviu wamefubaza makali ya ugonjwa huo.

Amesema, “tumeangalia ufanisi wa dawa tumefanya vipimo kwa wagonjwa 309,263, asilimia 96.6 ya waliofanyiwa vipimo wameonekana kwamba Virusi vya Ukimwi vimefubazwa.”

Unyanyapaa kwa watu wanao ishi na VVU – WAVIU, umekuwa ukirudisha nyuma juhudi za Kitaifa na Kimataifa za kutokomeza Maambukizi mapya ya VVU nchini ambapo inaaelezwa kuwa ARV ni suluhisho kwa WAVIU kupunguza uwezekano wa kuambukiza VVU kwa njia ya Ngono.

Dkt Kikwete aomboleza kifo cha Bernard Membe
Wataalam mradi wa LDFS wajadili taarifa usalama wa chakula