Bunge la nchini Ureno, imepitisha sheria ya kuhalalisha matumizi ya dawa ya euthanasia kwa watu walio katika mateso makubwa na magonjwa yasiyotibika huku upinzani mkali kuhusu matumizi ya dawa hiyo ukiibuka toka kwa Rais wa kihafidhina Marcelo Rebelo de Sousa.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya masharti ya dawa hiyo kutaka wale walio chini ya umri wa miaka 18 kutoruhusiwa kuitumia na wale walio na umri wa zaidi ya miaka 18 wataitumia ikiwa wapo kwenye hali mahututi.

Sheria hiyo itatumika tu kwa raia na wakazi halali na sio kwa wageni wanaokuja nchini kutafuta usaidizi wa kujiua huku muswada huo ukiidhinishwa na bunge kwa mara nne kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Hata hivyo, Rebelo de Sousa alikuwa amepinga miswada ya awali kutokana na dhana ambazo hazijafafanuliwa na baadaye akasema lugha inayotumika kuelezea hali ya wahusika iliendelea kukinzana na inahitaji kufafanuliwa.

Kisa Young Africans, Serikali yasogeza mbele
Simba SC yaahidi usajili mkubwa 2023/24