Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema maandalizi ya michuano ya Super League ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwaka huu, yanapaswa kuwa makubwa.

Super Cup ni mashindano yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ ambayo yanachezwa kwa mfumo wa ligi na jumla ya fedha za zawadi zitakuwa Dola za Marekani milioni 100, huku mshindi akipokea Dola za Marekani milioni 11.5.

Amesema michuano hiyo inakutanisha timu kubwa nane ambazo ni, Mamelod Soundown, Al Ahly, Horoya, Heart of Oak, TP Mazembe, Esperance, Wydad, Simba, na kuongeza unaweza kuona hata wale wapinzani wao wa Morocco yaani Raja Casablanca hawapo hivyo maandalizi yake yanapaswa kuwa makubwa.

“Kwa kuanzia kwenye usajili mzuri, benchi la ufundi, pre-season, ili kuweza kuendana na Super Cup, hivyo usajili utalenga kwenda kushindana na timu kubwa,” amesema Try Again.

Try Again amesema wanaangalia walipoangukia huko nyuma labda walifanya makosa, hivyo mapungufu waliyoyafanya wameyaona.

Aidha aliwaomba radhi wanachama, mashabiki na wapenzi kwa kushindwa kutwaa taji lolote ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo na kusema kwenye mpira hali hiyo huwa inatokea na hawapaswi kunyoosheana vidole badala yake kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

“Vitu vitatu vilivyochangia kukosa taji lolote msimu huu ni majeruhi kwa wachezaji wetu, nyota tuliowaongeza kushindwa kuonesha ubora pamoja na ugumu wa ligi kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi nachukua nafasi hii kuwaomba radhi Wanasimba wote, hatukuwa na msimu mzuri sababu tumekosa mataji yote,” amesema

Aishi Manula kupelekwa India
Mbunge ataka ufafanuzi kufungwa baa, sehemu za starehe