Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku ‘Musukuma’ ameomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni ya 76 akitaka kupata ufafanuzi juu  kufungwa kwa kumbi na sehemu za starehe kwa kigezo cha kuzidisha sauti huku akisisitiza kuwa hatua hiyo imeleta taharuki katika jamii.

Musukuma ameomba mwongozo wa Spika leo asubuhi jijini Dodoma akisema kuwa wananchi wengi hufanya kazi muda wote wa juma isipokuwa mwisho wa wiki ambapo huzitumia siku hizo hujiburudisha lakini kwa sasa maeneo ya starehe zikiwemo klabu katika majiji ya Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam zimefungwa.

Itakumbukwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Samuel Gwamaka alitangaza kuwa jumla ya baa na kumbi za starehe 89 zimefungiwa baada ya kubainika kuwa kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.

Aidha amesema kuwa mbali na maeneo hayo kutumika kuondoa msongo wa mawazo kwa wananchi, serikali inaingiza mapato hivyo kufungwa kwa kigezo cha kelele serikali inakosa makusanyo yake.

Amekwenda mbali na kulifananisha suala hilo na mgomo unaoendelea Kariakoo ambao umeibuliwa na Mbunge wa Makete, Festo Sanga mapema leo bungeni.

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo, Spika Tulia Ackson amesema Kanuni ya 76 inahusu jambo lililotokea Bungeni ‘Kwa hoja aliyoileta Musukuma, jambo hilo halipo katika kanuni hiyo ya Mwongozo,’ alisema Dk Tulia.

Hata hivyo Spika amelieleza Bunge kuwa mbunge huyo anaweza kuwasilisha hoja hiyo kupitia kanuni nyingine ikiwa anaona inafaa.

Try Again afunguka usajili wa CAF Super League
Chelsea, Pochettino mambo safi, kazi kuanza 2023/24