Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amekosoa wasifu wa hayati Bernard Membe uliosomwa bila kukitaja chama hicho ambacho Membe amewahi kukitumikia enzi za uhai wake.

Zitto amemekosoa wasifu huo mara baada ya kusomwa wakati wa zoezi la kuaga mwili wa kiongozi huyo lililofanyika jijini Dar es Salaam na kusema Membe alikuwa ni mwanachama wa ACT – Wazalendo na ni historia ni vyema ikawekwa wazi.

Amesema, “naongea kwa niaba yangu binafsi kama mtu ninaemfahamu Membe na pia kama kiongozi wa Chama ambacho ndugu maana yake numemsikia Jaji akiongea hapa hatuwezi kufuta historia Membe alikuwa mwanachama wa ACT Wazalendo.

Enzi za uhai wake, Benard Membe mbali ya kuwa mwanachama wa ACT pia aliwahi kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama hicho kabla ya mwaka 2022 kurejea tena Chama cha Mapinduzi CCM.

Kapombe: Ninabaki Simba SC, nina deni kubwa
Klopp aiweka kiporo Man City 2023/24