Madiwani Wilayani Tarime Mkoani Mara wameitaka Jamii kuepukana na Vitendo vya uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kulinda vya vya maji na mlima Tarime.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Bomani, wamesema ni jukumu la kila mmoja kulinda Mazingira pamoja na kutii sheria zilizowekwa.

Diwani viti maalum, Nuru Hotae akizingumza katika Kikao hicho alihoji ni kwa mini Watu wanaharibu mazingira katika mlima Tarime kwa kulima na kujenga wakati taratibu na Sheria zinajulikana bila hatua stahiki kuchukuliwa.

Hata hivyo, mmoja wa Wajumbe wa kamati ya mazingira ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maadili kata ya Turwa, Chacha Machugu alisema walifanya doria kwenye mlima huo na na baadhi ya Watu wameshachukuliwa hatua.

Pamba FC: Hatutarudia makosa Play Off
Inzaghi: Inter Milan inachukuliwa poa Ulaya