Shekhe Jassim amewasilisha ofa ya mwisho iliyoboreshwa zaidi katika jaribio lake la kuinunua Klabu ya Manchester United kutoka kwa familia ya Glazer, Shirika la Habari la PA, limeeleza.
Sheikh Jassim, Mwenyekiti wa Benki ya Kiislamu ya Qatar na mtoto wa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, na mpinzani wake Sir, Jim Ratcliffe walikuwa wamewasilisha ofa zao zilizotarajiwa kuwa za tatu na za mwisho kwa klabu hiyo mwezi uliopita.
Lakini huku kukiwa na Imani na kambi ya Ratcliffe, Sheikh Jassim ameongeza thamani ya ofa yake, ambayo kama hapo awali ni ya asilimia 100, kwani italipa madeni yote na inajumuisha mfuko tofauti unaoelekezwa kwa klabu na jumuiya zake.
Viongozi na wafanyakazi ndani ya Old Trafford wana hamu ya kupata ufafanuzi juu ya hali ya mauzo ambayo ilianza Novemba, mwaka jana wakati United ilitangaza bodi ilikuwa ikitafuta “njia mbadala” za kuimarisha ukuaji wa klabu, huku chaguo moja la mauzo likizingatiwa.
Sheikh Jassim alikuwa mmiliki mtarajiwa wa kwanza kuthibitisha hadharani wakati ofa yake ya ilipowasilishwa kwa mara ya kwanza Februari na hivi karibuni alijiunga na Ratcliffe, Mmiliki wa INEOS mzaliwa wa Manchester.
Robo ya kwanza ya mwaka ilitambuliwa hapo awali kama wakati muhimu katika mchakato ambao umevuma na kutishia kuficha shinikizo la United la kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tarehe ya mwisho ya Februari ilifuatiwa na tarehe ya mwisho ya Machi kwa wale walioendelea, na Raine Group, iliyoletwa kusimamia uuzaji, kisha kuuliza wahusika kwa zabuni yao ya tatu na ya mwisho mnamo Aprili 28, mwaka huu.
Mashabiki wa United wameweka wazi nia yao ya kutaka kuuzwa kikamilifu kwa klabu hiyo ili itoke miknoni mwa familia ya Glazers, ambao hawakuwa maarufu tangu walipoinyakua klabu hiyo mwaka 2005.