Afrika haina uhaba wa vituko. Waziri mmoja mwanamama aliwakilisha nchi yake kwenye kikao Mjini Dakar Senegal na akiwa hapo ikawa kajiwekea la Utaratibu ka kuiba vijiko, visu na nyuma kila wanapoenda restaurant. Breakfast anaiba, ‘lunch’ anafutika na dinner anakamilisha mzigo wa siku husika.
Bahati mbaya kwake mhudumu mmoja mwenye macho manne akawa anajiuliza hivi visu vinatowekaje kiaina? Na mbona ni Kila sehemu huyu mama anapokaa?
Akajiandaa na kisimu châke akarekodi Waziri anapokuwa kazini. Akishapakia mzigo anapenda kwanza chumbani Ku offload cargo ndio aende ukumbini kwenye kikao. Kiherehere yule akaongea na mhudumu wa chumba cha mheshiniwa wakafungua sanduku wakakuta nusu ya sanduku limejaa cargo. Akachikua picha na video. Akaunganisha na île alitomrekodi mheshiniwa akipakia cargo restaurant. Documentary ya kama dk 10 ikawa tayari.
Akamfuata supervisor wake kumweleza. Supervisor akamuuliza una ushahidi? Kiherehere akamuonyesha film ya Nollywood. Supervisor akamwambia “unajua mama ni Waziri? Kiherehere akamjibu “sijui ila Nina hakikaa ni mwizi”. Supervisor akamshauri amezee. Yule supervisor alihofu je Meneja atalichukuliaje suala lile?
Mkutano ukaisha Waziri akaondoka na cargo yake.
Kiherehere hakuridhika. Akatafuta gazeti la nchi aliyotoka Waziri. Akawaambia ana habari motomoto ila wamkatie tozo awape ushahidi. Gazeti likamtuma mwandishi wake Kwenda Dakar. Wakampa tozo yake akawapa mapicha na video.
Aliporudi kwao yéyé na mhariri wake wakakubaliana wafanye biashara. Wakamzukia Waziri na Kumwambia “ulipokuwa Dakar ulibeba cargo Haram”. Waziri akaonyesha ushahidi kiduchu na akawaahidi tozo. Sasa Siku ya kupokea tozo Waziri akaweka mtego. Mwandishi akadakwa na TAKUKURU Yao!
Huu mwaka wa 3 Mwandishi yupo Gerezani! Mhariri kuona picha lilivyo akasinyaa! hapo Mkuu wa nchi akafanya mabadiliko Waziri (Miss Cargo) akatemwa. Hakuna aliyejua katemwa kawaida au kwa kubeba cargo ya visu, vijiko na nyuma? Kama ndivyo si mwandishi angeachiwa?
Je kisa hiki cha kweli kinakufundisha nini?