Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali ametoa onyo kali kwa mpinzani wake kutoka Zambia, Simon Ngoma kwa kumwambia anatakiwa ajikaze kweli kwa kuwa amejipanga vizuri kwa kuhakikisha anafanikiwa kuibuka na ushindi katika pambano lake mwishoni mwa juma hili.

Pialali ametoa kauli hiyo kuelekea katika pambano la Classic Night linalotarajia kupigwa Mei 27, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Warehouse Masaki.

Pialali amesema kuwa bado anaendela na maandalizi ya kuelekea katika pambano hilo lakini ametoa angalizo kali kwa mpinzani wake kwa kumwambia atahakikisha anamchakaza katika hali yoyote kwenye pambano hilo.

“Binafsi naendelea vizuri na maandalizi ya pambano langu, namshukuru Mungu makocha wangu na timu yangu imekuwa ikinipa sapoti ya kutosha kuelekea katika pambano lenyewe pale Warehouse, kikubwa nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa sababu hili pambano kwangu naona ni sehemu ya kupasha misuli kuelekea Septemba katika pambano langu na Mfaume Mfaume.

“Lakini nataka nimwambie mpinzani wangu kuwa nimejipanga vizuri kwa sababu yake sina presha wala wasiwasi wowote, Ngoma namjua vizuri kwa sababu ameshakuja hapa sioni sehemu ambayo anaweza kunisumbua kwa sababu nimejipanga kuipa heshima nchi yangu.” amesema Pialali

Waziri akumbwa na kashfa wizi wa vijiko Hotelini
Mpango kukabili mabadiliko tabianchi waandaliwa