Benchi la Ufundi la Mtibwa Sugar limeanza hesabu za mchezo wa mzunguuko wa 29 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar, ili kufanikisha alama tatu muhimu zinapatikana

Mei 15, 2023 Mtibwa Sugar ilishindwa kufurukuta katika Uwanja wa Ushirika Moshi, Kwa kufungwa na Polisi Tanzania 3-1, hali ambayo iliifanya timu hiyo ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro kupoteze alama tatu mazima.

Kwenye msimamo Mtibwa ipo nafasi ya 14, ina alama 29 baada ya kucheza mechi 28 itakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya saba ikimiliki alama 35.

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Charles Ilanfya amesema kuwa wanafanya maandalizi kwa mechi zao zilizobaki, huku Benchi la Ufundi likiwa na hesabu kali za kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya Kagera Sugar.

“Kuna ushindani mkubwa na kila timu inahitaji kupata matokeo ambacho tunakifanya ni kuwa makini na kutumia muda tunaopata wa maandalizi kujipanga vizuri.

“Kila timu inahitaji matokeo nasi pia tunahitaji kupata ushindi kwenye mechi zetu na inawezekana.”

Ndani ya ligi Mtibwa Sugar ikiwa imefunga mabao 28, Ilanfya katupia mabao manne.

Ukicheza Aviator ya Meridian unapata bashiri 20 bure
Urusi yatangaza ushindi, Ukraine yaubeza kiaina