Bondia Idd Pialari amebadilishiwa mpinzani zikiwa zimesalia siku tatu na sasa atazipiga na Bryson Gwayan raia wa Malawi.

Awali Pialari alipaswa kupanda ulingoni kumkabili Simon Ngoma raia wa Zambia ambaye ameshindwa kufikia uzito aliotakiwa.

Pambano hilo la raundi nane lisilokuwa la ubingwa linatarajiwa kupigwa Jumamosi (Mei 27) kwenye Ukumbi wa Warehouse, Masaki Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Idd Pialari amesema kuwa anaendelea na maandalizi yake kama kawaida yeye kama bondia hachagui wa kucheza naye yuko tayari kumkabili yeyote ulingoni.

Hilo linakuwa pambano la 40 kwa Pialari ambaye ana rekodi ya kushinda michezo 30, sare moja na kupoteza mara nane wakati Gwayani amepanda ulingoni mara 23, ameshinda mara 14 na kupoteza mapambano tisa.

Aidha, hii ni mara ya pili kwa bondia Gwayani kuja nchini Tanzania mara ya mwisho alipoteza kwa pointi mbele ya Salim Jengo “Messi wa Ngumi” pambano lililofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Vijana watumie mafunzo ya JKT kujiajiri - Bashungwa
Serikali yapongeza ufanisi SUMA JKT