SUMA JKT, imeendelea kutekeleza shughuli za uzalishaji mali, biashara na huduma kupitia miradi na kampuni zake tanzu ikiwemo miradi ya ujenzi ya majengo ya Wizara na Taasisi za Serikali tisa katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Sambamba na hatua hiyo, SUMA JKT pia imeilitekeleza ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma, ujenzi wa majengo ya ofisi mbalimbali za Serikali, Idara, Vyuo na Taasisi binafsi katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai, 2022 hadi Aprili, 2023, na kufanya jumla ya miradi inayoendelea kutekelezwa kwa kipindi husika kufikia 210.

Hayo yamebainishwa, Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema, miradi miwili ya usambazaji wa umeme inayotekelezwa katika mikoa ya Morogoro na Shinyanga kupitia Mradi wa Rural Energy Agency (REA), kutoa huduma ya ushauri, ubunifu na usanifu majenzi, ambapo miradi 19 inaendelea kutekelezwa.

“Kuzalisha maji ya Uhuru Peak ambapo Kiwanda kimeongeza mikondo miwili ya uzalishaji wa maji kwa ujazo wa mililita 350 hadi lita 1.6 na lita 13 hadi lita 18, kuuza matrekta, zana za kilimo, vipuri vya matrekta na kutoa huduma baada ya mauzo. Huduma hizo zinatolewa katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Simiyu, Manyara, Katavi, Ruvuma, Kagera, Geita, Kigoma na Pwani,” amesema.

Aidha, amesema, “naomba nitoe wito kwa washirika mbalimbali wa maendeleo kushirikiana nasi katika sekta hii muhimu kwa ajili ya kukuza viwanda vyetu nchini, Pia, tunawakaribisha wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya kijeshi ili kuwezesha uzalishaji wa zana na vifaa vya kijeshi na hivyo kuipunguzia Serikali gharama za kuagiza kutoka nje ya nchi”, amesema

” Tuendelea kulijengea uwezo Jeshi la Kujenga Taifa kutoa mafunzo ya uzalendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa na stadi za kazi kwa vijana wa Mujibu wa Sheria na wa kujitolea na kuendelea kuimarisha Jeshi la Akiba”, amesema Waziri Bashungwa.

Iddy Pialali abadilishiwa mpinzani
Chino arudisha majibu kwa Ibrahim Class