Bondia Said Chino ametamba kuelekea pambano lake la ubingwa wa taifa unaotambulika Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), litakalorindima  katika Ukumbi wa Ware House, Dar es salaam Jumamosi (Mei 27), dhidi ya Ibrahim Class.

Bondia Chino amesema anaendelea vizuri na maandalizi ya pambano hilo na ana uhakika wa kushinda, kutokana na kumfahamu vizuri mpinzani wake.

“Nimejipanga vizuri kuhakikisha Chino hatoki salama siku hiyo, yule motto mdogo nitamuonesha ngumi zinavyochezwa,” amesema Chino akizungumzia pambano hilo

Hata hivyo Chino amesema hamuogopi mtu hivyo amewaomba mashabiki kuja kwa wingi kushuhudia atakachofanya.

Naye Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa amesema pambano hilo litakuwa la raundi 10 katika uzito wa Super feather, huku akithibitisha kutoa baraka zote.

Serikali yapongeza ufanisi SUMA JKT
Fiston Mayele afichua siri ya kambi Young Africans