Uongozi wa KMC FC umeweka wazi kuwa kikosi chao kitamaliza kwa heshima mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ambazo watacheza ugenini jijini Mbeya.
Mechi hizo mbili ambazo KMC FC imebakiwa nazo ni dhidi ya Tanzania Prisons Itakayochezwa Juni 6, kisha Juni 9 ni dhidi ya Mbeya City.
Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala, amesema maandalizi yapo sawa na wanatambua umuhimu wa mechi hizo zilizobaki.
“Tuna mechi mbili ngumu na za ushindani mkubwa, tunajipanga kwa ajili ya kupata matokeo mazuri na tunatambua haitakuwa kazi rahisi.
“Ukweli ni kwamba nafasi ambayo tupo ni ngumu na ili kubaki kwenye ligi ni muhimu kufanya vizuri kwa kupata pointi tatu, tunaamini itakuwa hivyo na mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Christina
KMC FC ina alama 29 baada ya kucheza mechi 28 kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.