Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi, Daniel Chongolo amepiga marufuku Mkoa wa Iringa kuwa sehemu ya kupata mabinti wa kazi na badala yake Mkoa wa Iringa usifike kwa kutoa mabinti wenye taaluma mbali mbali nchini.

Chongolo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi kijiji cha Wenda jimbo la kalenga katika ziara yake Mkoani Iringa na kusema kuwa ni aibu Mkoa wa Iringa kusifika kwa kutoa mabinti wa kazi za ndani.

Amesema, “Iringa sio mkoa wa kupata mabinti wa kazi badala yake watafute madaktari, wauguzi ,mainjinia na mabinti wenye taaluma mbalimbali,hivyo nawaomba wananchi kuhakikisha mabinti na vijana wote wanaenda shule.”

Aidha, ameongeza kuwa historia inaonyesha kuwa watu walikuwa wanatafuta mabinti wa kazi Mkoani hapo kwa sababu watu wa mkoa huo ni waaminifu”

“Kupitia uaminifu huo kwani hawawezi kiwa watu wenye taaluma mbalimbali waaminifu mpka wawe mabinti wa kazi? alihoji? Na kusema kuwa huo uaminifu wautumie kama daraja na kufanya mambo ya msingi kwa kuwasomesha watoto vizuri,” amesema.

Kesi ya Mchungaji Ezekiel: Mawakili waishutumu Idara ya upelelezi
KMC FC: Hatuna wasiwasi na alama 06 ugenini