Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amelaumu serikali ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kutopambana na biashara ya pombe haramu na dawa za kulevya nchini humo.

Akizungumza kwenye kikao na wadau jinsi ya kumaliza pombe haramu na dawa za kulevya katika Bonde la Ufa, Gachagua alisema kuwa wengi wamekuwa wakikashifu na kuilaumu serikali iliyopo madarakani lakini tatizo lilianzia awamu iliyopita.

Amesema, “hali hii ilidorora kabisa wakati wa serikali hiyo nyingine. Hawakujali hata. Watu waliuza pombe saa zisizostahili, wengine pombe haramu huku maafisa wakitazama tu. Lakini sitawalaumu maafisa. Hawakuongozwa inavyofaa.”

Hata hivyo, Bw Gachagua alisema wakati Rais William Ruto alichukua usukani, alitatizika na jinsi maafisa wote wa serikali kuu walivyotekeleza wajibu wao na kusema wengi walikuwa wameacha kazi zao na kujiunga na siasa.

“Kazi ya maafisa ni kuhakikisha kuwa kuna usalama, hakuna wizi wa mifugo, wauzaji na wapikaji pombe haramu wamekamatwa lakini wale waliokuwa serikalini walikuwa wamepewa majukumu ya kuokota saini za kuunga mkono BBI pamoja na kuuza sera za Azimio,” amesema Gachagua.

Cheza Mara Nyingi Kasino ya Mtandaoni Ushinde
Ramaphosa kuchunguza madai ya Marekani kuisaidia Urusi