Mamlaka za Marekani na Mexico zimelitaka Shirika la Afya Duniani kutangaza dharura ya afya ya umma kutokana na mlipuko wa fangasi ya uti wa mgongo unaohusishwa na shughuli za upasuaji wa urembo nchini Mexico.

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa – CDC, vilisema watu wawili waliopata upasuaji unaohusisha kuchoma ganzi ya kuzuia maumivu wamekufa kwa ugonjwa wa uti wa mgongo, na tayari Marekani imewatambua watu 25 wenye visa vya homa hiyo.

Takriban watu 400 nchini humo wanafuatiliwa ili kufahamu iwapo wameathiriwa na tatizo hilo ili kuweza kuchukua hatua stahiki za matibabu juu yao na tayari Kliniki mbili za vipodozi katika mji wa Matamoros nchini Mexico zimefungwa.

Mapema mwezi Oktoba 2022, kundi la dawa ya ganzi ya kawaida inayotumika kwa upasuaji, liligunduliwa kuwa imeambukizwa na fangasi ya aina hiyo na kusababisha vifo vya watu 39 katika jimbo la Durango lililopo nchini Mexico.

Kocha USMA atabiri mazito fainali ya pili Algeria
Askari wawili wauawa mbuga ya Wanyama