Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imemuhukumu Lionel Rayford raia wa Marekani kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha kilo 2.188.

Hukumu hiyo imetolewa Mei 26, 2023 na Jaji Isaya katika shauri la uhujumu uchumi namba 17 la mwaka 2021.

Raia huyo wa Marekani alikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Julai 5, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, wa Julius Nyerere akiwa ameficha dawa hizo katika moja ya mabegi aliyokuwa nayo.

Madai Polisi kuuwa raia sita: IPOA yaanza uchunguzi
Wenye ulemavu wanatengwa, wanabaguliwa - Othman