Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa imesema itachunguza madai ya Marekani kwamba kuna meli ya Russia iliyochukuwa silaha kutoka katika kambi ya wana maji karibu na jiji la CapeTown mwaka 2022.

Nchi hiyo, ilikanusha shutuma hizo ambazo zimesababisha malumbano ya kidiplomasia miongoni mwa Marekani, Afrika Kusini na Russia, na kuhoji msimamo wa Afrika Kusini wa kutoegemea upande wowote kwenye mgogoro wa Ukraine.

Katiha hali nyingine, waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov amesema ahadi ya baadhi ya mataifa ya Magharibi kuipatia Ukraine ndege za kivita aina ya F-16, haikubaliki na ameyashutumu mataifa hayo kwa kuidhoofisha Russia.

Lavrov amesema, hatua hiyo ni kucheza na moto na kwamba Wizara ya Mambo ya nje ya Russia imekuwa ikisisitiza juu ya kutojihusisha na hatua hiyo ambayo imesema ni hatari.

Gongo, Dawa za kulevya: Gachagua amshushia lawama Kenyatta
Bola Tinubu aapishwa rasmi kuwa rais wa Nigeria