Gavana wa Mkoa wa Darful uliopo Magharibi mwa Sudan, Mini Minawi amewahimiza raia kwenye eneo hilo kubeba silaha ili kujilinda na wahujumu wa taasisi za taifa.

Amesema, raia wanapaswa kuchukua silaha kulinda mali zao dhidi ya watu wasiotaka usalama au haki za umma wa Sudan ili kujiweka salama na kulinda familia zao.

Hata hivyo, Darfur imekuwa na vita vita ya muda mrefu tangu mwaka 2003 na katika mapigano yanayoendelea sasa vifo na majeruhi vimeshuhudiwa pia kwenye eneo hilo.

Minawi ambaye ni kiongozi wa zamani wa kundi la waasi, amesema kwa upande wake analiunga mkono jeshi la taifa linalopambana na kikosi cha wanamgambo wenye nguvu cha RSF.

Askari wawili wauawa mbuga ya Wanyama
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 29, 2023