Waziri wa Nishati, Januari Makamba Serikali ipo katika mikakati kwa kipindi cha ndani ya miaka miwili suala la Umeme liwe ni historia hapa Nchini.
Makamba ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Media Bungeni kwenye maonyesho ya Wiki ya Nishati na kuongeza kuwa ni kweli suala la Umeme bado halijatengemaa lakini kupitia mpango huo litamalizika.
Amesema, “Kwanza tumepiga hatua kubwa, lakini binafsi sijafika pale nilipokua napatamani kwenye maboresho yanayotakiwa kufanyika, Tunamshukuru Mheshimiwa Rais ametupa nafasi ya kuboresha sekta hii.”
Kuhusu uzalishaji wa umeme nchini, Waziri Makamba amesema umeongezeka kwa asilimia 11 kwa mwaka, ambapo awali kulikua ongezeko la asilimia 5 kwa mwaka jana (2022), na kwa mara ya kwanza wanakaribia kuongeza asilimia 10.
“Watu wanalalamika kukatika umeme Rais Samia ametupatia Trilion 1.9 ya kufanya miradi 26 na miradi hio imeanza, bei ya mafuta imeshuka. Tumezima tayari baadhi ya maeneo yaliyokua yanazalisha umeme wa Dizeli,” amesema Makamba.