Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, amesema kuwa wanafanyia kazi makosa ambayo waliyafanya kwenye mechi zilizopita ili kumaliza vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.
Kagera Sugar inatarajiwa kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mcheza ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro, Juni 6, mwaka huu.
Kocha Maxime amesema mechi za kumalizia msimu ni muhimu kupata ushindi ili kuwa na mwisho mzuri.
“Matokeo kwenye mechi huwa yanakuja kutokana na mchezo husika unaweza kufanya maandalizi mazuri kabla ya mchezo ila siku ya mchezo hali ikawa tofauti.
“Hakuna mchezaji ambaye hapendi kupata matokeo mazuri na sisi tunafanya kila kazi kutafuta ushindi na mwisho dakika 90 zinatoa matokeo kwenye mchezo husika.” amesema Maxime