Waziri wa Nishati, January Makamba amesema kutokana na mipango ya Serikali, ifikapo mwezi Juni mwaka 2024 vijiji vyote Tanzania vitakuwa na umeme.
Makamba amesema Serikali ina mipango inayozingatia utabiri wa hali itakavyokuwa mbeleni, lakini pia inaishirikisha zaidi sekta binafsi katika kuwekeza kwenye sekta ya nishati ili kuweza kufikia malengo kwa wakati.
“Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere tulibadilisha ratiba, sasa hivi kazi inafanyika usiku na mchana, siku za wkend na sikukuu, zamani ilikua ikifika saa 12 jioni watu wamefunga, hio ndio siri ya mradi kukimbia kwenye ujenzi wake,” amesema Makamba.
Wizara ya Nishati, inatarajia kuwasilisha bungeni makadirio ya bajeti yake ya mwaka wa fedha 2023/2024 kuanzia siku ya Jumatano May 31 2023.