Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema, tafiti zinaonesha kuwa katika vikwazo vya utumiaji wa gesi ya mitungi, uwoga wa gharama unalingana na ule wa kudhani mitungi inaweza kulipuka.

Makamba ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na Kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Media Bungeni kwenye maonyesho ya Wiki ya Nishati na kuongeza kuwa kitendo cha kiongozi wa Serikali kwenda kugawa mitungi kwa wananchi kinatuma ujumbe kwamba mitungi ile ni salama.

Amesema, “tukizungumzia gesi ya mitungi, kulikuwa na vikwazo viwili kwa watuamiaji, cha kwanza ni gharama ya awali ya mtungi wenyewe, pili ni uwoga kwamba mtungi unaweza kulipuka,”

Hata hivyo, Waziri Makamba amesisitiza kuwa Serikali itafanya mambo ya kibajeti na kikodi, ili kupunguza gharama ya gesi ya kupikia nchini.

Try Again, Robertinho watoa kauli za kibabe
Azam FC yajimwambafai safari ya Tanga