Kuelekea mchezo wa Mzunguuko wa 29 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe, amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kupambania alama tatu.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unatarajiwa kupigwa Juni 06, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Ibwe amesema: “Zimebaki takribani siku saba tushuke dimbani kucheza mchezo wetu dhidi ya Coastal Union, kikosi kinaendelea na maandalizi kabla ya kuelekea Tanga huku hali na morali ya wachezaji ikiwa nzuri kabisa.

“Coastal Union ni timu yenye historia kubwa na sisi kwa sababu imekuwa ni moja ya timu ambayo inatuonesha upinzani mkubwa sana ndani ya uwanja.

“Benchi la ufundi limeshafanya tathmini ya kutosha kuhusu wapinzani wetu na nina imani kuwa tutafanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo huu pamoja na mechi yetu ya mwisho kumaliza msimu dhidi ya Polisi Tanzania.”

Mitungi ya Gesi ni salama - Makamba
Kesi ya Mchungaji Ezekiel: Mawakili waishutumu Idara ya upelelezi