Mahakama ya Shanzu iliyopo jijini Mombasa nchini Kenya, imesikiliza kesi ya Mhubiri tata wa kanisa la Good News International, Paul Mackenzie ambapo upande wa mashtaka umeomba aendelee kuzuiliwa kwa siku 60 zaidi.

Upande huo wa mashtaka unataka mhubiri huyo, mkewe na watu wengine 16 waendelee kuzuiliwa wakati uchunguzi ukiendelea kufuatia madai ya .Mackenzie na wenzake kupotosha waumini na kupelekea kufunga hadi kufariki.

Aidha, inadaiwa kuwa waumini hao walishawishika kufunga na wakaanza kufariki miili yao ilipodhoofika huku uchunguzi wa madktari ukibaini wengine waliochelewa kufa waliuawa.

Hadi kufikia sasa, miili ya watu zaidi ya 243 imeshafanyiwa upasuaji katika mochwari ya Hospitali Kuu ya Malindi iliyopo katika Kaunti ya Kilifi na ripoti zimekuwa zikijulishwa kila mara.

Arsenal kurudi tena kwa Moises Caicedo
Wawili KMC FC kusubiri hadi 2023/24