Uongozi wa klabu ya Brighton unaamini Arsenal itakuwa na pesa inayotosha kumsajili kiungo inayemsaka kwa nguvu zote, Moises Caicedo ambaye bei yake ni Pauni 75 milioni.

Arsenal ilifanya jaribio la kumsajili mkali huyo wa Ecuador kwenye dirisha la Januari, lakini Brighton iligoma kabla ya sasa kuweka milango wazi ya kumpiga bei katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi kama itawekwa pesa ya maana mezani.

Kinachoelezwa ni kwamba mabosi wa Brighton wanataka Pauni 75 milioni kwenye mauzo ya kiungo huyo na kuwaambia Arsenal kama watakuwa tayari kutoa mkwanja huo, basi watafanikiwa katika mpango wao wa kupata huduma ya kiungo huyo matata.

Arsenal inahitaji pia huduma ya nahodha wa West Ham United, lakini saini ya kiungo huyo Mwingereza, Declan Rice inatajwa ni kubwa zaidi, si chini ya Pauni 100 milioni na hapo itabaki kwa Kocha Mikel Arteta kuamua ni saini ya mchezaji gani kati ya hao wawili atapenda kuinasa kwanza.

Kocha Arteta anataka kutengeneza kikosi chake kuwa cha kibabe kuhakikisha kinaonyesha ushindani mkali wa mataji kwa msimu ujao, huku akitambua wazi watakuwa kwenye kasheshe la kukabiliana na vigogo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufuzu kucheza michuano hiyo msimu ujao.

Kwenye Ligi Kuu England msimu wa 2022/23, Arsenal ilimaliza nafasi ya pili, ikipigwa kikumbo na Manchester City kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo licha ya kuongoza kwa asilimia 90 ya msimu.

Kuhusu Caicedo shida inabaki kwa Arsenal kama watakuwa tayari kulipa kiasi hicho.

Ihefu FC yatamba kuirarua Geita Gold
Vifo mfungo tata: Upande wa mashtaka waomba siku 60 zaidi