Uongozi wa Ihefu FC umesema kuwa mpango wao mkubwa kuelekea mchezo wa mzunguuko wa 29 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya dhidi ya Geita Gold FC, ni kupata alama tatu muhimu.

Ihefu FC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo katika  Uwanja wa Higland Estate, Mbeya Juni 6, mwaka huu.

Afisa Habari Ihefu, Peter Andrew amesema: “Tupo kwenye lala salama na kila timu inahitaji kupata matokeo hilo benchi la ufundi linatambua na mpango ni kuona kwamba tunapata ushindi.

Wawili KMC FC kusubiri hadi 2023/24 

“Tukiwa nyumbani tunakuwa na furaha kwani mashabiki wengi wamekuwa wakijitokeza hilo linawapa nguvu wachezaji kucheza kwa juhudi kutafuta ushindi tunaamini itakuwa hivyo kwenye mchezo wetu ujao,”

Ikulu yatafafanua kilichomuangusha Rais jukwaani
Arsenal kurudi tena kwa Moises Caicedo