Ripoti ya waandishi wa Habari wa Ikulu ya White House nchini Marekani, imesema Rais wa nchi hiyo Joe Biden alianguka baada ya kujikwaa kwenye mfuko mweusi wa mchanga alipokuwa akipanda jukwaani.

Biden alianguka alipokuwa akikabidhi cheti cha Diploma katika sherehe ya kuhitimu kwa Chuo cha Jeshi la Wanahewa la Marekani kilichopo Colorado.

Biden, ndiye rais mkongwe zaidi wa taifa hilo akihudumu nafasi yake akiwa na umri wa miaka 80, mara baada ya kuanguka alisaidiwa kusimama na alionekana kuwa hajadhurika ingawa alikuwa akichechemea.

Awali, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu ya White House alisema Rais alikuwa amesimama kwa takriban saa moja na nusu kupeana mikono na kila mmoja wa wanafunzi 921 waliohitimu chuo hicho.

Erling Haaland: Tunalitaka taji la Ulaya
Ihefu FC yatamba kuirarua Geita Gold