Serikali nchini Kenya, imepokea msaada wa tani 34,000 za mbolea kutoka Russia, ambao unalenga kuimarisha kilimo kwa ajili ya usalama wa chakula.

Akizungumza mjini Mombasa, baada ya kuipokea meli iliyobeba shehena ya mbolea Waziri wa kilimo, Mithika Linturi amesema hatua hiyo itaboresha kilimo na hivyo kuhakikisha usalama wa chakula nchini humo.

Alisema, “Wakulima wamenunua zaidi ya magunia milioni 2.8 ya mbolea katika majimbo 34 nchini Kenya na mbolea hii tuliyoipokea itatusaidia kuwafikia wakulima zaidi walio katika maeneo mengine nchini humu.”

Msaada huo, utatumiwa kutengeneza tani laki moja za mbolea aina mbali mbali, kisha kuwauzia Wakenya katika mpango unaoendelea wa kuwapa wakulima mbolea kwa bei nafuu.

Simba SC yapigwa bao Afrika Kusini
Wafanyabiashara wajishitaki Serikalini, DC achukua hatua