Mawakili wa Serikali nchini, wametakiwa kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano na usuluhishi, ili kutengeneza mazingira mazuri yatakayowavutia wawekezaji kuwekeza nchini.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bi.Mary Makondo ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Amesema, Mawakili wa serikali wanatakiwa kuhakikisha wanatumia mafunzo hayo kwenda kuongeza ufanisi katika taasisi zao na kusaidia kupungunza migogoro na mrundikano wa kesi mahakamani kwa njia ya majadiliono.

“Nchi ikiwa na migogoro,kesi na matukio yasiyofaa hakuna maendeleo hivyo serikali inatambua kazi kubwa mnayoifanya ila kaongezeni kasi ya utatuzi wa migogoro ili kuwavutia Wawekezaji,” amesema Bi.Mary Makondo.

Joash Onyango: Azam FC imetuvurugia Simba SC
Waziri Mbarawa awasilisha maelezo ya awali mkataba TPA