Mwanamke mmoja anayeishi Rongai, Kaunti ya Kajiado nchini Kenya, amewaua watoto wake wawili na kisha kumdunga kisu mumewe na kujaribu kujitoa uhai kwa kujichoma na kisu kifuani katika ugomvi ambao bado haujafahamika chanzo chake.

Kwa mujibu wa Polisi walipofika eneo la tukio, wamesema walimkuta mume wa mwanamke huyo akiwa amelala chini huku akivuja damu nyingi huku miili ya watoto hao wawili wenye umri wa miaka 6 na 2 ikikutwa sakafuni.

Aidha, inadaiwa kuwa mwanamke huyo alikutwa akiwa amejinyonga kwa nyuzi huku akivuja damu na kisu hicho kikiwa kifuani ambapo Poliosi hao walimkimbiza yeye na mumewe Hospitali wakiwa katika hali mbaya.

Miili ya watoto hao baadaye ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti na Polisi walisema waliitwa na majirani ambao inaonekana walimsikia mwanamke huyo akipiga kelele kuomba msaada baada ya kujaribu kujitoa uhai kwa kutumia kisu hicho.

Pep Guardiola: England hawaisapoti Man City
Tottenham yamuwinda Harry Maguire