Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote juu ya muda wa miaka 100 wa uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam kupitia Kampuni ya DP World kutoka Falme za Kiarabu kama inavyoenezwa.

Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na maneno mengi juu ya uwepo wa mkataba wa kampuni hiyo kuwekeza bandarini kwa miaka 100 – jambo ambalo limezua taharuki.

“Wakati huu ambao Chadema itatoa taarifa kuhusiana na sakata hili, mimi kwa maoni yangu binafsi nasema kuwa sijaona mahali popote kunapoonyesha kuwa Kampuni ya DP World wamepewa ofa ya miaka 100 ya kuendesha Bandari yetu,” Alisema Lissu

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini Tanzania (TPA), jana usiku walilazimika kutoa taarifa kwa Umma, juu ya uwapo wa kikundi cha watu walioamua kwa makusudi kupotosha kuhusiana na mchakato wa maboresho ya Bandari nchini yenye lengo la kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Utatu mtakatifu kuibukia Newcastle Utd?
Usajili 2023-24: Wawili waivuruga Geita Gold FC