Mabosi wa Newcastle United huenda wakapiga mchongo na klabu za Saudi Arabia wanazochezea mastaa Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Karim Benzema ili kuwanasa kwa mkopo wakakipige St James’ Park msimu ujao.

Hakuna sheria ya kuwazuia Newcastle United isifanikiwe kumnasa mmoja wa mastaa hao kwa mkopo.

Kampuni ya Saudi Arabia Public Investment Fund inayomiliki asilimia 80 ya klabu ya Newcastle United, juzi ilizinunua klabu kubwa kabisa nne za kutoka taifa hilo la Kifalme.

Al-Ittihad, Al-Ahli, Al-Nassr na Al-Hilal zote zitakuwa chini ya kam- puni inayomilikiwa kwa asilimia 75 na PIF.

Supastaa Ronaldo anakipiga Al-Nassr na Benzema amesaini mkataba wa miaka miwili huko Al-Ittihad.

Wakati mchezaji huru Messi ikisemekana baba yake anamtaka aende Barcelona, lakini kuna ofa ya pesa ndefu kabisa imetoka Al-Hilal inamtaka staa huyo wa Kiargentina kwa zaidi ya Pauni 350 milioni.

Timu hizo chini ya umiliki wa klabu hizo zinaweza kufanya biashara ya kupeana wachezaji na hilo PIF wanataka kulifanyia kazi.

Hata hivyo, inatazamiwa kuwapo na upinzani mkali kutoka kwa klabu za Ligi Kuu England kama Newcastle itajaribu kuleta huduma ya mastaa hao kwa  gharama nafuu.

Mmiliki mwenza wa Newcastle, Jamie Reuben alisema ili kuweka mambo sawa katika kuepuka kukiuka udhibiti wa matumizi ya pesa basi watafanya kazi zao katika weledi mkubwa.

Hakuna ukomo wa idadi ya wachezaji unaoweza kuwa nao kwa mkopo kwenye Ligi Kuu England kwa wale wa kutoka ng’ambo na Newcastle wanaweza kutumia hilo kama fursa na kuwa na mastaa wote watatu kwenye kikosi chao Ronaldo, Benzema na Messi endapo kama atanaswa na moja ya klabu za Saudi Arabia.

Victor Lindelof apeta Manchester United
Lissu: Mkataba wa DP Bandarini si wa Miaka 100