Serikali nchini, imesema itaendelea kutekeleza kikamilifu Ilani ya Chama cha Mapinduzi – CCM, kwa yote yalioahidiwa ikiwemo suala la wananchi kupata huduma bora za afya, huku ikiwataka Wananchi kutoa taarifa pale wanapobaini matukio ya wizi wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tabora inayogharimu shilingi Bilioni 2.8 iliopo katika kata ya Mpela mtaa wa Uledi Manispaa ya Tabora.

Amesema, “Wananchi mnatakiwa kutoa taarifa pale mnapobaini matukio ya wizi wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya, lakini Watumishi pia mtunze miundombinu iliowekwa pamoja na kuwahudumia wananchi kwa upendo na kutumia taaluma zenu kuokoa Maisha.”

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais pia amekemea vikali tabia ya kukiuka taratibu za manunuzi na kuwataka watumishi wa umma kuhakikisha wanazingatia sheria katika taaluma zao.

Usajili 2023-24: Wawili waivuruga Geita Gold FC
Wizara ya Fedha yaomba Bunge kuidhinisha Trilioni 15