CHAMA cha Walimu Tanzania – CWT, kimemsitisha Katibu Mkuu, Japhet Maganga kutoendelea na shughuli za Chama, baada ya kutotimiza wajibu wake na kuvunja kanuni na katiba ya chama huku baadhi ya watendaji wa chama hicho wakizuiwa kuingia kazini kutokana na ubadhilifu.

Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Jijini Dodoma, Muwakilishi wa Walimu Mkoa wa Njombe wa kamati ya utendaji wa Taifa, Thobias Sanga amesema hatua hiyo inatokana masuala ya fedha kwenda kinyume na uwepo wa baadhi ya viongozi nje ya taasisi kwa muda mrefu.

Amesema, “sisi tumejiridhisha na tumeona kazi zetu haziendi sawa pamoja na kazi zetu za utendaji haziendi kama katiba na kanuni zinavyosema, na mahamuzi yetu kama Watendaji na wanachama tumeazimia katibu Mkuu hatoendesha shughuli za Chama kuanzia leo.”

Aidha Sanga ameongeza kuwa, “hatumsimamishi ukatibu Mkuu ila tunamsimamishia shughuli zake alizokuwa anafanya kwenye taasisi na badala yake shughuli hizo hatafanya Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho.” amesema Sanga

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Joseph Misalaba amesema hajapendezwa na suala la wafanyakazi kuwazuia viongozi wao kutoingia ofisini na kuwafungia geti ambapo hali hiyo imezuwa taharuki kwa wapita njia.

Amesema, “niseme tu kuwa hali hiyo ni ukosaji wa nidhamu, japo kuwa hatukupata taarifa kuwa kuna viongozi watafika ofisini lakini haikutakiwa hali hii kufikia hapa.”

Mbeya: Wananchi waiomba Serikali kutatua kero zao
Gundogan aidengulia Manchester City