Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi chana amesema miongoni mwa sababu zilizochangia kutofikiwa malengo ya kazi za sanaa ni kutokana na wadau wengi wa filamu kufanya kazi zao bila ya kufuata utaratibu wa kisheria ikiwemo kukosa vibali na kuingiza filamu sokoni kabla ya kuhakikiwa.

Dkt. Chana ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa sababi nyingine ni kuchelewa kukusanywa na kugawanywa kwa mirabaha ya kazi za wabunifu na kwa upande wa vyuo, moja ya sababu ni wanavyuo kutokulipa ada kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali.

Aidha, Dkt. Chana ameongeza kuwa, “katika mwaka wa fedha 2022/23, Wizara iliidhinishiwa bajeti yenye jumla ya Shilingi Bilioni Thelathini na Tano, Milioni Mia Nne Ishirini na Tano, Mia Tisa Tisini na Moja Elfu (Sh. 35,425,991,000) ambapo kati ya hizo Mishahara ilikuwa Shilingi Bilioni Nane, Milioni Mia Mbili na Moja, Mia Nane Themanini na Mbili Elfu (Sh. 8,201,882,000).”

Amesema, “matumizi mengineyo ni (OC) shilingi Bilioni Kumi na Moja, Milioni Mia Tatu Tisini na Mbili, Mia Tisa Arobaini na Tisa Elfu (Sh. 11,392,949,000) na Miradi ya Maendeleo (DEV) Shilingi Bilioni Kumi na Tano, Milioni Mia Nane Thelathini na Moja, Mia Moja Sitini Elfu (Sh. 15,831,160,000).”

Gundogan aidengulia Manchester City
Andy Cole: Man Utd bado sana kutwaa ubingwa