Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Deogratius Ndejembi amezitaka Halmashauri za Miji na Majiji nchini kuhakikisha kuwa maeneo yote yanayopangwa kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya wananchi na kuwekewa miundombnu muhimu ya kijamii na kiuchumi.

Ndejembi ameyasema hayo wakati akizungumzia zoezi la usafi wa mazingira, katika sehemu ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Juni 5, 2023 Jijini Dodoma ma kuongeza kuwa pia wanatakiwa kuhakikisha maeneo hayo kwa sasa yanawekewa utaratibu wa kupandwa miti, ili kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Amesema, “Halmashauri hazina budi kuhakikisha kuwa mnapopima viwanja maeneo hayo pia yapandwe miti, ili kuwezesha miji yote kuendelea kuwa ya kijani. Tusipime viwanja na kuwaachia wakazi wenyewe, tuna wajibu wa kuhakikisha barabarani zetu zinapandwa miti.”

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alisema Mkoa wa Dodoma umeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika utunzaji na uhifadhi na utunzaji wa mazingira ikiwemo kuwahamasisha wananchi kujumuika katika kufanya usafi wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Amesema, Ofisi yake inatambua kuwa Serikali imeipa Dodoma sura tofauti katika suala la usafi wa mazingira na ambapo Mkoa huo tayari umeweka mikakati mbalimbali ya kulinda na kuhifadhi mazingira na kuanzia katika ngazi mbalimbali ikiwemo shule, taasisi na jamii kwa ujumla.

Agizo: Kila kaya iwe na sehemu ya kuchomea taka - Dkt. Mpango
Vipaumbele Nishati: Upo uzalishaji, usambazaji wa umeme