Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania – TAWA, imewaonya wote wanaojihusisha na vitendo vya ujangiri wa wanyama pori katika hifadhi na mbuga za Wanyama nchini, kuacha kazi hiyo mara moja huku ikisema vitendo hivyo kwasasa vimepungua.

Rai hiyo, imetolewa na Ofisa Mhifadhi Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama pori Tanzania – TAWA, Proches Rongoma wakati wakishiriki maonyesho ya 10 ya Biashara na Utalii yanayofanyika mkoani Tanga.

Afisa mhifadhi mwandamizi – TAWA, Proches Rongoma.

Amesema, “suala au kitendo chochote cha kuuchukua mali ya wanyama pori bila kibali ni ujangiri na ujangiri upo wa aina tofauti, wa kibiashara na wa chakula, kuna watu wanao uwa wanyama kwa ajili ya chakula na kwaajili ya kufanya Biashara, Watanzania wajue kwamba wao ndio wahifadhi wa kwanza wa wanyama pori.”

Awali, Afisa Mhifadhi daraja la pili kutoka Mamlaka hiyo, Veronica Mollel aliwasisitiza na kuwahimiza watanzania kuendelea kufanya utalii wa ndani katika hifadhi mbalimbali zilizopo nchini , ili kujionea vivutio na kujifunza amali mbalimbali zilizopo.

Dante awachimba mkwara askari magereza
Polisi Tanzania: Simba SC hawataamini macho yao