Klabu ya Tottenham ipo kwenye mchakato wa kuweka mambo sawa kwa ajili ya kumpata nahodha wa Klabu ya Manchester United, Harry Maguire.

Maguire bado hatma yake ndani ya Man United haijafahamika kwani beki huyo kwa sasa anataka kuona akicheza ili kujihakikisha nafasi katika timu ya Taifa ya England.

Imeelezwa kuwa, mchakato wa kumtaka Maguire umeanza hivi karibuni baada ya kutangazwa kwa meneja mpya wa Tottenham anayefahamika kama Ange Postecoglou.

Maguire amekuwa sio chaguo la kwanza katika kikosi cha Erik ten Hag eneo la mabeki wakati mpaka wakati mwingine kulazimika kumchezesha Luke Shaw ambaye ni beki wa kushoto.

Beki huyo inaelezwa anaweza kuondoka hapo na itakuwa rahisi kutokana na uwepo wa Harry Kane ambaye wamekuwa pamoja katika timu ya Taifa ya England.

Maguire alisajiliwa na Man United kwa dau la rekodi kiasi cha Pauni 80m kutoka katika Klabu ya Leicester City.

Wakati Tottenham wao wakimpigia hesabu Maguire, Man United nao wanamtolea macho Kane ambaye kwa sasa pia anaangaliwa na Real Madrid kama mbadala wa Karim Benzema.

Mama auwa watoto wake kwa kisu, amjeruhi mumewe
Dkt. Tulia awashukia wapotoshaji ukodishaji Bandari