Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia ackson amekanusha taarifa zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii kuwa Bunge limeridhia makubaliano ya uendelezaji wa bandari.

Dkt. Tulia ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma na kusisitiza kuwa azimio la suala hilo lipo katika ngazi ya kamati ya pamoja.

Amesema, “kumekuwepo na upotoshaji kuhusu suala la Bandari ya Dar es Salaam naomba na ninaomba kutokea ufafanuzi wake unaolenga kuepusha upotoshaji uliojitokeza wakati Serikali inaenda kuboresha bandari zetu.”

Hapo jana, Juni 7, 2023 Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, alisema hakuna ukweli wowote juu ya muda wa miaka 100 wa uwekezaji kwenye Bandari ya Dares Salaam kupitia Kampuni ya DP World kutoka Falme za Kiarabu kama inavyoenezwa.

Tottenham yamuwinda Harry Maguire
Watatu kuondoka Azam FC 2023/24