Takriban watu zaidi ya 40 wamefariki katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, baada ya Wanamgambo wenye silaha wa kundi la CODECO kushambulia kambi ya wakimbizi katika jimbo la Ituri.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Afisa Tawala wa Bahema Badjere – Djugu, Richard Dheda na Mwakilishi wa mashirika ya kiraia, Desire Malodra wamesema wanamgambo hao walianza kufyatua risasi na watu wengi waliteketea kwa moto katika nyumba zao huku wengine wakiuawa kwa mapanga.

Mkoa wa Ituri umekuwa ukikabiliwa na vitendo vya ghasia na mauaji – CODECO, au Ushirika kwa ajili ya Maendeleo ya Kongo, ni kundi linalodai kulinda jamii ya Lendu dhidi ya jamii ya Wahema, na pia dhidi ya jeshi la Kongo.

Elimu sauti zilizozidi viwango ni muhimu - Dkt. Gwamaka
Serikali kutafuta muafaka athari zitokanazo na sauti