Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amevishauri vyama vya ushirika Mkoani Kagera kufanya maboresho ikiwemo kununua kahawa sawa na bei na wanunuzi binafsi wa nchi jirani na kuhakikisha wakulima wanapatiwa malipo yao ndani ya saa 24 baada ya kuuza kahawa yao.

Mwasa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa vyama vya ushirika Mkoani Kagera, katika jukwaa la maendeleo ya ushirika ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza mkoani humo katika ukumbi wa mikutano wa Bukobacop ulioko mjini Bukoba.

Amesema, “mkulima yeye ahangalii ni nani ananunua bei nzuri anataka apate faida ya kilimo chake, biashara ni ushindani hapa tulipo ni mpakani mkoa jirani tunaopakana nao wananunua kahawa na ni wauzaji wa Kahawa na sisi tunanunua kahawa kesi kubwa iliyopo hapa ni kuondoa utoroshaji wa kahawa.”

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa.

Aidha ameongeza kuwa, “sasa tusikubali sisi tunatoka jasho kwa kulima alafu wengine wanauza Ulaya na Marekani kwa bei kubwa na kufanya takwimu zao zinaonyesha kiwango cha juu cha uuzaji lakini wao si wakulima haya ni masuala ya msingi kukubaliana, kuyazungumza, kuelewana na kuyafanyia kazi.”

Hata hivyo Mwassa amebainisha kuwa, “si busara wakulima wanapaswa waeleshwe waelewe wanapotorosha kahawa kupeleka kule wanajipa hasara wenyewe kwani ata ile malipo ya ushuru wa huduma ambayo ingesaidia kujenga zahanati, viti vya wanafunzi na huduma nyingine yote tunaipoteza.”

Picha: Ujenzi daraja la Magufuli wafikia asilimia 75
Arsenal yakaribia usajili wa Declan Rice