Idadi ya vifo vya waumini wa Muhubiri tata Paul Mackenzie nchini Kenya imeongezeka hadi kufikia watu 303 ikiwa ni miezi miwili baada ya kufichuliwa kwa kisa hicho ikidaiwa kuwa imesababishwa na mafundisho ya kiimani kuwa watu hao wafunge hadi kufa ili kukutana na Muunba wao.

Zoezi la kutafuta na kufukua makaburi ya halaiki bado linaendelea katika Msitu huo wa Shakahola, uliopo karibu na mji wa Pwani wa Malindi, ambapo waathiriwa wa kwanza baadhi yao walifariki na wengine kukutwa hai lakini wakidhoofika kiafya.

Mmoja wa wafuasi wa mhubiri tata Paul Mackenzie akishindwa kutembea mara baada ya kufikishwa Mahakamani Shanzu hii leo Juni 14, 2023.

Polisi nchini humo imesema inaamini kwamba miili mingi iliyofukuliwa ni ya waumini wa Kanisa la Kimataifa la Habari Njema (Good News International Church), dhehebu la kiinjili lililoundwa mwaka wa 2003 na mchungaji huyo, Paul Nthenge Mackenzie.

Uchunguzi wa maiti umefichua kuwa wengi wa waathiriwa walikufa kwa njaa, na kwamba pia baadhi ya wahanga wakiwemo watoto walinyongwa, kupigwa au kukosa hewa.

Mawakili wawili wajitoa kesi ya Mhubiri tata Paul Mackenzie
Nyaraka za siri USA: Trump akana mashitaka